Je, mgeni anahitaji kupakua app?
Hapana. Mgeni anafungua kiungo alichotumiwa kwa WhatsApp au SMS, na kadi inafunguka kwenye kivinjari cha simu yake. QR yake ipo pale pale kwa ajili ya mlangoni.
Vipi kama mgeni hana WhatsApp?
Anapata ujumbe wake kwa SMS. Kwa kila kundi tunakuonyesha ni wangapi wana namba ya simu kabla hujatuma, ili usibaki na mtu ambaye hakufikiwa.
Kadi moja inaweza kubeba watu wangapi?
Unaamua mwenyewe — mtu mmoja hadi sita kwa kadi. Mlangoni tunahesabu wanaoingia, kwa hiyo familia inayofika kwa nyakati tofauti inaingia bila ubishi.
Nani anafanya kazi ya kuscan siku ya tukio?
Unaweza kutengeneza akaunti za wasaidizi wako mwenyewe — wanaona skrini ya kuscan pekee, si orodha ya wageni wala malipo. Ukipenda, tunaweza kukuletea wasaidizi wetu kwa gharama ya ziada.
Nikifuta mgeni, nimepoteza pesa yangu?
Hapana. Kadi uliyolipia inabaki kama salio kwenye tukio lako, na unaweza kumpa mtu mwingine bila kulipa tena.
Je, ni harusi tu?
Hapana. Sendoff, kitchen party, mahafali, kumbukumbu, Eid, ibada, makongamano, matamasha ya tiketi na matukio ya kampuni — kila aina ina miundo yake ya kadi na vitufe vyake.
Ninauzaje tiketi za tamasha langu?
Unaweka aina za tiketi na bei zake, kisha unasambaza kiungo kimoja cha mauzo. Mnunuzi hahitaji akaunti wala app — analipa kwa simu, na tiketi yenye QR yake inamfikia. Langoni unascan, na tiketi iliyotumika haipiti mara ya pili. Fedha zinaingia kwenye salio lako, unatoa wakati wowote.
Kanisa au kongamano hufanyaje bila orodha ya majina?
Kiungo ni kimoja kwa wote. Anayefungua anajiandikisha mwenyewe kwa jina lake, na ndani anaona mpangilio wa ibada, matangazo, ushuhuda na mifuko ya sadaka. Tukio linalipiwa mara moja badala ya kwa kila kadi.
Naweza kulipa kwa cash?
Ndiyo. Mkikubaliana bei, msimamizi anaisajili kwenye mfumo na huduma inafunguka — kadi, salio la ujumbe au vifaa. Malipo ya cash yanaonekana kwenye ripoti zako kama cash, si kama pesa iliyopita mtandaoni.
Malipo yanafanyikaje?
Kupitia ClickPesa — M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halopesa na kadi. Kadi zinafunguka zenyewe mara malipo yanapothibitishwa; si lazima uburudishe ukurasa.