AsanteSanaAnza bure

ZANA YA BURE

Template ya orodha ya wageni

Safu zilizoandaliwa kwa jinsi orodha inavyotumika siku ya tukio — si tu majina, bali kundi la kila mgeni na watu wangapi kadi yake inabeba.

Pakua template

Jaza kwenye Excel au Google Sheets, kisha ubandike moja kwa moja kwenye AsanteSana — hakuna kuandika upya.

Safu zilizomo, na kwa nini

Safu ya “watu kwenye kadi” ndiyo watu husahau — na ndiyo huleta ubishi mlangoni siku ya tukio.

Jina kamiliKama litakavyoonekana kwenye kadi
Namba ya simu0712 345 678 au +255 712 345 678
KundiFamilia, Marafiki, VIP, Wafanyakazi
Watu kwenye kadi1 kwa mtu mmoja, 2 kwa mume na mke
UpandeBibi harusi au bwana harusi
MaelezoMahitaji maalum, mzio wa chakula

Mfano

Jina kamiliNamba ya simuKundiWatu kwenye kadiUpandeMaelezo
Amina Msuya0712 345 678Familia2Bibi harusi—
John Mrema0754 612 338Marafiki1Bwana harusi—
Dkt. Rehema Mgaya0687 231 009VIP2Bibi harusiKiti cha mbele
Godfrey Mushi0748 338 121Wafanyakazi1Bwana harusi—

Ukimaliza kujaza

  1. 1Fungua akaunti ya AsanteSana na utengeneze tukio lako.
  2. 2Kwenye ukurasa wa wageni, bonyeza “Pakia orodha”.
  3. 3Bandika safu za Jina, Simu na Kundi. Kila mgeni anapata kadi na QR yake.

Orodha ikishakuwa tayari, iliyobaki ni kazi ya dakika

AsanteSana inatengeneza kadi ya kila mgeni, inapanga meza kwa makundi, na inatuma kwa WhatsApp na SMS. Kadi 10 za kwanza ni bure.

Anza bure